Home VIWANDAMIUNDOMBINU Kipaumbele cha kwanza ni kujenga miundombinu: Rais Mwinyi

Kipaumbele cha kwanza ni kujenga miundombinu: Rais Mwinyi

0 comment 130 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Ali Mwinyi amesema matarajio yake kwa sasa ni kujenga miundombinu kwanza.

Akihutubia katika maadhimisho ya miaka miwili ya kuiongoza Zanzibar, Rais Mwinyi amesema “kipaumbele cha kwanza katika miaka miwili ijayo ni kujenga miundombinu mikubwa, miundombinu ya barabara kuu katika nchi yetu.

Miundombinu ya bandari kubwa Unguja na Pemba, miundombinu ya viwanja vya ndege vya kisasa, na ninapata faraja kwa sababu tayari haya yote ninayoyasema yapo katika mchakato yanakaribia kuanza.”

Amesema Bandari ya Mangapwani itakuwa bandari ya aina yake na itabadilisha uchumi wa Zanzibar.

“Bandari za Pemba sasa zitakuwa bandari za kisasa ambazo meli kubwa zitakuja moja kwa moja sio zile meli zinashusha kwanza Unguja halafu ndo ulete huku mzigo,” amesema.

Amesema miaka miwili inayokuja hatua za maendeleo zitakuwa kubwa zaidi kuliko iliyopita.

Amebainisha kuwa kiuchumi kwa sasa wapo pazuri kuliko walivyoingia.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter