Meneja uhusiano wa kampuni ya mabasi yaendayo haraka (Udart)Deus Bugaywa amesema mgomo wa wafanyakazi wa kitengo cha kukata tiketi umepelekea kampuni hiyo kukosa mapato yanayokadiriwa kuwa kati ya Sh. 70 milioni na Sh. 90 milioni kwa siku kutokana na huduma za usafiri huo kutolewa bure.
Bugaywa amesema japokuwa kampuni imepata hasara kubwa, walifikia uamuzi wa kutoa huduma ya usafiri bure kutokana na kutambua umuhimu wa safari za abiria wao na pia kwa heshima ya mradi huo ambao unatambulika na kusifika kimataifa.
Mgomo huo wa wakata tiketi umesababishwa na kucheleweshwa kwa mishahara yao ya April na Mei hali ambayo imepelekea zaidi ya watu 70,000 jijini Dar es salaam kusafiri bure kuanzia Ijumaa iliyopita.