Home VIWANDAMIUNDOMBINU Madaraja matatu kujengwa Gairo

Madaraja matatu kujengwa Gairo

0 comment 101 views

Kufuatia uharibifu wa madaraja matatu ya Chakwale, Nguyami, na Matale wilayani Gairo kutokana na kusombwa na maji ya mafuriko, serikali imepanga kutoa fedha za dharura wilayani humo ili kukarabati madaraja matatu ambayo yanaunganisha wilaya ya Gairo na wilaya ya Kilindi Tanga, ili kuondoa changamoto ambazo wakazi wa mikoa hiyo wamekuwa wakikumbana nazo, hususani suala la usafirishaji.

Akizungumza na  wananchi wa kijiji cha Nguyami wilayani humo, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Isack Kamwelwe amewaahidi wananchi hao kufuatilia suala hilo kwani hali halisi  inaonekana na mabadiliko yanatakiwa kufanyika haraka iwezekanavyo.

“Tutatumia fedha ya dharura kujenga madaraja ya mita 50 hadi 60 katika mto Chakwale, Nguyami na Matale ili maji yaweze kupita chini na yakijaa kupita juu yake bila kuliathiri daraja lililojengwa, haya yatakuwa ni madaraja ya dharura”. Amesema Waziri huyo.

.Naye Mbunge wa jimbo hilo, Ahmed Shabiby, amesema kuwa Rais Magufuli aliwaahidi kutengeneza barabara hiyo wakati wa kampeni, hivyo utekelezaji huo utawafurahisha wakazi wa wilaya hizo na kuimarisha uchumi pamoja na mawasiliano kati ya Morogoro na Tanga.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter