Home VIWANDAMIUNDOMBINU Ufaransa kuisaidia Tanzania ujenzi wa miundombinu

Ufaransa kuisaidia Tanzania ujenzi wa miundombinu

0 comment 111 views

Ufaransa imesema ipo tayari kusaidiana na Tanzania katika ujenzi wa bandari itakayohudumia Tanzania na nchi jirani.
Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa, Chrysoula Zacharopoulou amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.Mwigulu Nchemba.
“Ufaransa ipo tayari pia kutusaidia kukuza sekta binafsi ambayo imekuwa ikitoa ajira nyingi kwa vijana nchini”, ameeleza Dkt. Nchemba.

Ameongeza kuwa Serikali ya Ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha miundombinu ya barabara, nishati na umeme wa jua ili iweze kutumika katika shughuli za uzajilishaji.

Naye Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, amesema kuwa Ufaransa imetangaza rasmi kushirikiana na Tanzania katika kukuza sekta ya utalii kwa kuwa ina mchango katika pato la Taifa.

Ameongeza kuwa Serikali ya Ufaransa imekuwa ikiisaidia Zanzibar katika kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo miundombinu, afya na nishati.

Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo na Ushirikiano wa Kimataifa wa Ufaransa Chrysoula Zacharopoulou, amesema kuwa pamoja na ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Ufaransa, anaamini kuwa bado kuna mengi zaidi ya kushirikiana kati ya nchi hizo mbili.


Zacharopoulou alipongeza msimamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwenye masuala ya jinsia na nia ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Jukwaa la Usawa wa Kizazi (Generation Equality Forum) baadae mwaka huu.

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter