Home FEDHA Huduma za Kifedha kuwafikia wazalishaji vijijini

Huduma za Kifedha kuwafikia wazalishaji vijijini

0 comment 47 views
Na Mwandishi wetu

Ili kumaliza tatizo la wazalishaji wadogo vijijini kutofikiwa na huduma za kifedha kwa ukamilifu, halmashauri 73 hapa nchini zimeanza utekelezaji wa mpango maalum unaolenga kuimarisha uwezo wa vyama vya ushirika, vikundi vya wasindikaji na wazalishaji wadogo pamoja na asasi ndogo za kifedha vijijini.

Mkurugenzi wa Taasisi Endelevu ya Elimu ya Ushirika ya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU) Jastin Bamanisa amesema mpango huo upo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia program ya Miundombinu ya Masoko, Uongezaji wa Thamani na Huduma za Kifedha Vijijini (MIVARF), na chuo hicho kimetengewa kiasi cha Sh. 3 bilioni ili kutekeleza mradi huo.

Bamanisa ameongeza kuwa mpango huo utafikia asasi za kifedha 1,200 na SACCOS zisizopungua 200 pamoja na Benki ya Wananchi. Pia watendaji katika asasi hizo ndogo wameanza kujengewa uwezo huku akisistiza kuwa mpango huu utafanikiwa kwa kiasi kikubwa na kuwapa walengwa matokeo yenye tija kwani lengo kubwa la serikali ni kuongeza kipato na uhakika wa chakula huku gharama za utafutaji wa soko na upatikanaji wa huduma za fedha vijijini zikipungua.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter