Home VIWANDAMIUNDOMBINU Ujenzi wa bandari Pwani wamvutia Kamwelwe

Ujenzi wa bandari Pwani wamvutia Kamwelwe

0 comment 136 views

Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe amesema ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa bandari kavu ya Kwala mkoani Pwani. Waziri Kamwelwe amesema hayo baada ya kutembelea mradi huo unaotekelezwa na Suma-JKT na kueleza kuwa, bandari hiyo inatarajiwa kuanza kupokea mizigo rasmi Julai Mosi 2019 na kuwa suluhisho kwa changamoto ya kuondoa mizigo iliyopo katika Bandari ya Dar es salaam hususani inayosafirishwa kuelekea Rwanda, Uganda, Malawi, Zambia, Congo, Burundi na nchi nyingine za maziwa makuu. Vilevile, Waziri huyo amesema kuwa, bandari hiyo itahusisha pia miundombinu ya reli, barabara na majengo kwa ajili ya ofisi na kutoa huduma mbalimbali.

“Kukamilika kwa bandari kavu kutaongeza kasi ya upakuaji mzigo kwa meli zinazoingia Dar es salaam kwani moja ya changamoto sasa katika bandari hiyo ni ufinyu wa eneo la kuweka makasha”. Amesema Waziri huyo.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Usimamizi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Deusdedit Kakoko amesema kukamilika kwa mradi huo ambao hadi sasa umegharimu Sh. 15 bilioni kutaiwezesha kupokea na kutunza makasha zaidi ya milioni 1.5 tofauti na hali ilivyo sasa ambapo eneo la bandari linachukua makasha 650,000 pekee.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter