Serikali imetenga kiasi cha Sh bilioni tisa kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa fukwe ya kisasa ya Coco maarufu kama Coco beach. Akizungumzia mradi huo, Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amesema mradi huo ambao unatarajia kuanza siku za hivi karibuni na utaiweka fukwe hiyo ambao wakazi wengi wa jiji la Dar es salaam na mikoa mingine huitumia kwa ajili ya mapumziko katika mandhari nzuri fukwe na kutoa wito kwa watanzania zaidi kufika kwenye maeneo hayo.
Amesema serikali imeamua kubadilisha Dar es Salaam kuwa jiji la kisasa na la kibiashara hivyo fukwe za Coco zimerudishwa serikalini ili kufungua milango kwa wanachi wote kuzitumia. Makonda pia ameeleza kuwepo kwa miradi mingine ya uboreshaji wa jiji kuanzia kwenye makazi ya watu pamoja na miundombinu ya barabara.