Home VIWANDAUZALISHAJI Mwijage aeleza sababu za kushindwa kufikia malengo uzalishaji wa sukari

Mwijage aeleza sababu za kushindwa kufikia malengo uzalishaji wa sukari

0 comment 74 views

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage amesema Tanzania imeshindwa kufikia malengo ya tani 314,000 za sukari na badala yake kuzalisha tani 300,399 kutokana na ukame uliozikumba nchi za ukanda wa mashariki, kati na kusini mwa bara la Afrika. Mwijage amesema hayo wakati akiwasilisha bajeti ya wizara hiyo bungeni Dodoma ambapo pia ameeleza kuwa mahitaji ya sukari kwa mwaka hapa nchini ni tani 630,000 na kati ya hizo, tani 485,000 ni kwa matumizi ya kawaida huku tani 145,000 zilizosalia zikiwa ni kwa ajili ya matumizi ya viwandani.

Mwijage amezitaja kampuni nne ambazo zimepewa jukumu la kuagiza sukari kutoka nje ya nchi kuwa ni Kilombero, Kagera, TPC pamoja na Mtibwa. Kampuni hizo zinabeba jukumu la kuhakikisha hakutokuwa na upungufu wa sukari hapa nchini na zimetakiwa kupanua mashamba yao ya miwa hadi kufikia mwaka 2020 ili kuwezesha nchi kujitosheleza na bidhaa hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter