Home VIWANDANISHATI Njombe kuzalisha umeme wa upepo

Njombe kuzalisha umeme wa upepo

0 comments 212 views

Mradi wa umeme wa upepo unategemewa kuanzishwa mjini Makambako mkoa wa Njombe chini ya kampuni iitwayo Windlab Development Tanzania. Mradi huo uliopewa jina la Miombo Hewani Wind Farm utazalisha megawati 300 kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza ya mradi huo itawanufaisha takribani wakazi milioni moja wa mjini Makambako.

Mkurugenzi Mtendaji wa Windlab Development Tanzania Katherine Persson amesema kuwa mradi huo utakapokamilika utadumu kwa miaka 25 hadi 30. Pia wanafanya kila jitihada kuhakikisha wakazi wa vijiji vya Igomba, Isimike na Itengero wananufaika na mradi huo.

Hata hivyo Bi. Persson amesema kuwa makubaliano kuhusu eneo yameshafanyika na mradi huo wa Dola za Marekani 250 milioni utachukua muda wa miezi 12 hadi 18 kukamilika. Pia umeme huo utauzwa  Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa bei nafuu.

“Ili kuzalisha megawati 100 za kwanza inahitaji mitambo ya upepo 34 na vilevile miundombinu ya umeme itakayounganisha shamba la upepo kwenda kwenye gridi ya taifa ya umeme katika kituo cha Makambako”. Amesema Mkurugenzi huyo.

Pia ameongeza kuwa mradi huo utakuwa na hisa kubwa kutoka milioni 10 za kimarekani. Mwaka jana kampuni hiyo ilipata cheti cha tathmini ya mazingira na jamii iliyopo karibu na eneo ambalo mradi huo utaanzishwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!