Home VIWANDAUZALISHAJI CSTC kuteka soko la muhogo

CSTC kuteka soko la muhogo

0 comment 167 views

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kulima na kusindika muhogo ya Cassava Starch of Tanzania Corporation (CSTC), Christophe Gallean amewaambia waandishi wa habari kuwa wanatarajia kuzalisha takribani tani 6,000 za unga wa muhogo kwa mwaka. Gallean ameeleza kuwa kiwanda hicho kitazalisha tani moja za unga wa muhogo kwa siku huku kikisafirisha katika masoko muhimu duniani kama vile Marekani, Afrika Mashariki na Kusini, Ulaya na Mashariki ya Kati.

“Tunafurahi kuanzisha rasmi kiwanda cha kwanza cha ubora wa hali ya juu na cha kisasa nchini Tanzania. Tunajivunia sana uwepo wa kiwanda hiki na taswira inayoipa kampuni yetu ya CSTC, Mkoa wa Lindi na Tanzania kwa ujumla. Tunashukuru sana kwa ushirikiano wa serikali chini ya uongozi wa Rais John Magufuli. Mfumo wa utendaji wa CSTC ni kukuza mazao yenye ubora wa hali ya juu katika mashamba makubwa yenye ufanisi na kusimamiwa na CTSC. Vilevile kusindika mazao yote katika kiwanda kilichopo eneo la karibu, mfumo huu wa utendaji unaofuatwa na CTSC wa kuzalisha mazao na kuwa na kiwanda cha usindikaji ni wa kipekee katika soko la unga wa muhogo wa Afrika”. Ameeleza Gallean.

Kiwanda hicho kilianzishwa miaka saba iliyopita kwa lengo la kuuza unga wenye ubora ndani na nje ya nchi. CSTC ilianza kufanya kazi rasmi mwaka 2012 ikiwa na wafanyakazi wapatao 400, asilimia 97 wakiwa watanzania.

“Tunaendelea kuongeza wafanyakazi, kutoa mafunzo na kuendelea kutoa fursa kwa vijana wengi za uongozi katika ngazi zote za uendeshaji kuanzia kiwandani, mashambani na katika shughuli za utawala”. Amesema Mkurugenzi huyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter