Home WANAWAKE NA MAENDELEO Fursa ya aina yake kwa wanawake

Fursa ya aina yake kwa wanawake

0 comment 118 views

Benki ya DTB imepanga kufungua tawi maalum jijini Dar es salaam,ambapo wafanyakazi watakuwa wanawake pekee. Meneja Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Teknolojia wa benki hiyo, Stella Masha ameeleza hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani na kueleza kuwa, DTB imekuwa mstari wa mbele katika masuala ya usawa ndio maana wamejipanga kufungua tawi ambalo huduma zote zitatolewa na wanawake.

“Wito ni kuzingatia usawa wa kijinsia ulimwenguni na kaulimbiu ya siku ya wanawake kwa mwaka huu ni; Kuzingatia usawa katika jamii zetu. Ulimwengu ulio sawa kijinsia ni ulimwengu bora zaidi”. Amesema Meneja huyo.

Aidha, Masha pia ameeleza kuwa benki ya DTB inaunga mkono harakati za usawa wa kijinsia na katika utoaji ajira, wamefanikiwa kufanya hivyo, ikiwa asilimia 49.1 ya walioajiriwa ni wanawake. Pamoja na hayo, asilimia 50 ya waajiriwa kwenye matawi ya jijini Dar es salaam ni wanawake.

“Pia tupo katika mipango ya kufungua tawi maalum lenye wafanyakazi wanawake pekee Dar es salaam kabla ya mwisho wa mwaka huu, kwa kuwa tumeona mafanikio yao na ubora wao katika utendaji kazi wao. Tunapenda kuwapa fursa wanawake na ndio maana nguvukazi yetu tunawapa wanawake kipaumbele”. Amesema.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter