• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Tuesday, October 3, 2023
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

Waziri Mkuu akutana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la China

“Tunaishukuru Serikali ya China kwa sababu tumepokea misaada na mikopo ya gharama nafuu na kuendeleza miradi mbalimbali"

Patricia Richard by Patricia Richard
November 17, 2018
in UWEKEZAJI
0
Waziri Mkuu: Utawala bora muhimu

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa.

Share on FacebookShare on Twitter

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameishukuru Serikali ya China kwa kuunga mkono jitihada za maendeleo zinazofanyika nchini hivi sasa chini ya uongozi wa Serikali ya awamu ya tano. Ametoa shukrani hizo jana jioni (Ijumaa, Novemba 16, 2018) alipokutana na Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China, Bw. Cai Dafeng ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

“Tunaishukuru Serikali ya China kwa sababu tumepokea misaada na mikopo ya gharama nafuu na kuendeleza miradi mbalimbali kama vile mradi wa umeme wa Kinyerezi, awamu ya pili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar,” alisema.

ADVERTISEMENT

Alisema Serikali ya China imekuwa pia na mahusiano ya muda mrefu na Serikali ya Tanzania na hasa kwenye sekta ya afya ambapo kuna wanafunzi wengi wa kitanzania ambao wako China wakisomea udaktari na masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA).

“Tuna mahusiano mazuri kwenye sekta ya afya na sasa hivi tuna madaktari 20 ambao wanasoma huko na wengine wanasomea masuala ya TEHAMA. Pia tuna mahusiano mazuri baina ya Bunge la Tanzania na China,” alisema.

Waziri alisema Tanzania imejipanga kuinua uchumi wake kupitia ujenzi wa viwanda na sekta nyingine kama utalii kutokana na vivutio vilivyopo nchini kama vile Mlima Kilimanjaro, mbuga za wanyama za Serengeti na visiwa vya Zanzibar. “Nimefurahi kusikia kuwa hivi karibuni tutapata idadi kubwa ya watalii kutoka China,” alisema.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Watu wa China, Bw. Cai Dafeng alisema amefurahishwa na jinsi Serikali ya awamu ya tano inavyoendelea kubadili hali ya uchumi wa nchi na maisha ya watanzania chini ya uongozi wa Dkt. John Pombe Magufuli.

Alisema China itaendelea kuiunga mkono Tanzania kwenye masuala ya kiuchumi na haiko tayari kuona ikiingiliwa masuala yake ya ndani na mataifa kutoka nje.

Akizungumzia kuhusu masuala ya uwekezaji baina ya Tanzania na China, Bw. Cai alisema China itaendelea kuyahimiza makampuni ya nchi hiyo ili yawekeze zaidi nchini Tanzania kwenye maeneo mbalimbali kama vile ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. “China inatarajia kuongeza uwekezaji kwenye kilimo, nishati na miundombinu,” alisema.

Kuhusu elimu, Bw. Cai alisema Serikali ya nchi hiyo inaangalia uwezekano wa kuanzisha masomo ya lugha ya Kichina katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili watanzania wengi zaidi waweze kujifunza lugha hiyo.

Kuhusu afya, alisema China itaendelea kutuma madaktari wake ili waje kutoa huduma kwa watanzania na inatamani kuona mahusiano baina ya mtu mmoja mmoja kutoka nchi hizo mbili ikiendelea kukua.

IMETOLEWA NA:

OFISI YA WAZIRI MKUU,

JUMAMOSI, NOVEMBA 17, 2018.

Tags: ChinaKassim MajaliwakilimomikopomiundombinuTehama
Patricia Richard

Patricia Richard

Next Post
Matajiri wanatumiaje pesa zao?

Uelewa wa takwimu kuchochea maendeleo

Discussion about this post

Habari Mpya

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki.

Wadau ufugaji nyuki watakiwa kuchangamkia fursa

September 14, 2023

Exim kulinda maslahi watumiaji huduma za bima

September 26, 2023
Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande.

Tanzania yapiga hatua utakatishaji fedha

September 12, 2023
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan. Picha| Ikulu

Tutawaunganisha wakulima na soko: Rais Samia

September 11, 2023

Mbaazi yaleta neema kwa wakulima 2023

September 7, 2023

Bei za mafuta zapanda tena Tz

September 6, 2023

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Waziri wa Maliasili na Utalii Angellah Kairuki.

Wadau ufugaji nyuki watakiwa kuchangamkia fursa

by Pesatu Reporter
September 14, 2023
0

Tanzania ni nchi ya pili kwa uzalishaji wa asali barani Afrika na inashika nafasi ya 14 dunia. Ethiopia, ndio nchi...

Exim kulinda maslahi watumiaji huduma za bima

by Pesatu Reporter
September 26, 2023
0

Benki ya Exim imezindua ushirikiano wa kimkakati na Mamlaka ya Udhibiti wa Bima Tanzania (TIRA) pamoja na kufanya mafunzo ya...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2023 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In