Home WANAWAKE NA MAENDELEO Mgodi wa wanawake wachangia Shilingi Milioni 800

Mgodi wa wanawake wachangia Shilingi Milioni 800

0 comments 61 views

Mgodi wa Dhahabu wa Manda, unaomilikiwa na wakinamama umechangia Shilingi Milioni 800 katika maduhuli ya Serikali kwa mwaka huu wa fedha 2024/2025.

Mgodi huu, ambao kwa kiasi kikubwa unaendeshwa na wakinamama, upo katika Kijiji cha Mwime, Kata ya Zongamela, Kahama. Una leseni ya uchimbaji mdogo wa madini na umeajiri zaidi ya vijana 200.

Afisa Madini Mkazi wa Kahama Leons Welengeile, amesema kuwa mgodi wa Manda ni miongoni mwa wadau muhimu na unatoa ajira kwa vijana na kinamama wengi kupitia shughuli zinazoendelea katika mgodi huo.

Alieleza kuwa kwa mwaka huu wa fedha, mgodi huu umechangia Shilingi Milioni 810 katika maduhuli ya Serikali, kupitia mrabaha na tozo ya ukaguzi ambazo zinakusanywa na Tume ya Madini Kahama, na makusanyo mengine yaliyokusanywa na halmashauri na TRA.

Kwa upande mwingine, Leons alisisitiza kuwa maduhuli ya Serikali katika Mkoa wa Kimadini Kahama yameendelea kupanda mwaka hadi mwaka.

Alitaja makusanyo ya Shilingi Bilioni 97 mwaka 2022/2023, Shilingi Bilioni 101 mwaka 2023/2024, na hadi kufikia Machi 2025, Shilingi Bilioni 88.08 zimekusanywa, ambayo ni sawa na asilimia 85 ya makusanyo ya miezi 9.

Leons pia alisisitiza kuwa kwa mwelekeo huu, anatarajia kuwa lengo la makusanyo litatimizwa ifikapo mwishoni mwa mwaka.

Asha Msangi, ambaye ni mmiliki wa mgodi huo na pia Mwenyekiti wa wanawake wachimbaji, anasema kuwa kabla ya kuanza shughuli za uchimbaji, alifanya biashara ndogo ndogo, lakini aliona changamoto na kuamua kuhamia kwenye uchimbaji madini.

Aliomba leseni ya uchimbaji na akaanza kwa majaribio, kisha alifanya vizuri na kuaminika hadi sasa anamiliki leseni 12. Aidha, Asha ameunda vikundi vya wanawake wachimbaji na anashirikiana nao katika shughuli za uchimbaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter

Subscribe my Newsletter for new blog posts, tips & new photos. Let's stay updated!