Home WANAWAKE NA MAENDELEO Mwongozo wa uwekezaji wa hisa kwa wanawake

Mwongozo wa uwekezaji wa hisa kwa wanawake

0 comment 94 views

Ni dhahiri kuwa wanawake hukabiliwa na vikwazo tofauti na vile wanavyokumbana navyo wanaume wakati wa kuwekeza katika masoko ya hisa. Mara nyingi huwa wanakuwa na akiba ndogo kutokana na kutumia muda mwingi kulea watoto, kutunza familia na kutoajiriwa kwa muda mrefu.

Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wengi huona ni afadhali wawekeze fedha zao katika benki au katika uwekezaji mwingine kuliko kuwekeza katika masoko ya hisa. Mtazamo huu sio mzuri sana kwani wanawake wengi duniani wamefanikiwa kutokana na uwekezaji wa hisa.

Watu wengi hawapendelei kuwekeza katika hisa kutokana na uoga wa fedha zao kupotea ikiwa soko litashuka ghafla. Na wengi hufanya biashara hizo kwa kusikiliza hisia zao ndio maana huwa inakuwa ngumu watu wengi kufanya uwekezaji huo na kufanikiwa. Badala yake, wanahifadhi fedha zao katika benki na sehemu nyingine bila kujua kuwa bado wanapoteza fedha nyingi huku kwa sababu hazizunguki. Inaelezwa kuwa uwekezaji wenye hatari kubwa siku zote huleta faida kubwa.

Kama muwekezaji katika soko la hisa ni muhimu kutambua kuwa lazima soko litashuka, hali hiyo hutokea kwa muda mfupi na utapoteza fedha. Hivyo ndivyo soko linavyofanya kazi. Bei zinaweza kubadilika vibaya lakini kwa kipindi kirefu mambo hubadilika na kuwa katika mwenendo mzuri kwa ujumla.

Hisia ni adui yako mkubwa katika uwekezaji wa hisa, unaweza kuona ni rahisi kusubiria muda mrefu hadi pale soko litakapokuwa na mwenendo mzuri lakini kwa matendo hiyo si kazi rahisi kwasababu hakuna mtu asiyependa kupoteza fedha zake na kifupi lazima hisia ziathiriwe ikiwa mtu husika kapoteza fedha. Tengeneza mpango kabla ya kuwekeza ili kupata muongozo hasa pale soko linaposhuka.

Wekeza, usifanye biashara. Kwa urahisi ni kwamba kufanya biashara maana yake muhusika anakuwa anauza na kununua fedha ili kuepuka kupata hasarana kujipatia mapato ya juu mara nyingi hii hufanya kazi mara chache. Hivyo kama unalenga kuwekeza hutakiwa kuwasikiliza watu wengine ikiwa watasema soko limepanda hivyo uuze hisa zako.

Kuhusu ada ya uwekezaji jitahidi kulipia ada yenye gharama nafuu kwani siku zote ada na uwekezaji haviingiliani na haimaanishi kuwa ukilipa ada kubwa ndio utapata mrejesho mkubwa.

Mwisho wa siku, ikiwa utajifunza misingi ya uwekezaji basi utakuwa na uwezo wa kufanikiwa katika uwekezaji kwa asilimia 90. Kwasababu utaondoa hofu na uoga uliokuwa nao mwanzoni. Kipindi soko litakaposhuka hapo ndio utajua uwezo wako wa kustahimili katika uwekezaji huo.

 

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter