Home WANAWAKE NA MAENDELEO Wanawake kupata mafunzo na mitaji wezeshi

Wanawake kupata mafunzo na mitaji wezeshi

0 comment 92 views

Benki ya CRDB imesaini makubaliano ya kushirikiana na taasisi za BUTA Vicoba Endelevu na Open Mind and Thoughts Organization (OMTO) kuwawezesha wanawake kupata mafunzo na mitaji wezeshi kupitia program ya IMBEJU.

Akizungumza kwenye hafla ya makubaliano hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB Bank Foundation, Tully Esther Mwambapa amezishukuru taasisi hizo kwa utayari wao wa kushirikiana na CRDB Bank Foundation katika program ya IMBEJU.

Aidha, Tully amewakaribisha wabia wengine kushiriki katika programu hiyo ili kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini.

Katika hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya CRDB, taasisi ya CRDB Bank Foundation pia ilikabidhi msaada wa Shilingi Milioni 10 kwa taasisi ya BUTA Vicoba Endelevu kwa ajili ya semina maalum kwa wanawake wajasiriamali inayotarajiwa kufanyika mwezi huu wilayani Newala, mkoani Mtwara.
Tully amewataka wanawake kote nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa kupitia program hiyo kukuza na kuboresha biashara zao.

Dirisha la maombi ya uwezeshaji kwa wanawake wajasirimali katika vikundi kupitia programu ya IMBEJU bado lipo wazi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter