Home WANAWAKE NA MAENDELEO Wanawake wahimizwa kuchangamkia mikopo

Wanawake wahimizwa kuchangamkia mikopo

0 comment 117 views

Ofisa Maendeleo ya Jamii mkoani Arusha, Irene Materu ametoa wito kwa wanawake katika Halmashauri hiyo kuacha tabia ya kuwa tegemezi kwa wanaume na kuwashauri kutumia fursa ya mikopo inayotolewa na Halmashauri kujikwamua kiuchumi. Materu amesema hayo wakati akizungumza na vikundi vya wanawake wajasiriamali na kuongeza kuwa, mikopo hiyo ni kwa ajili ya kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo.

“Ufike wakati sasa wanawake tukatae kuwa tegemezi, tujikwamue kiuchumi kwa ajili ya kutunza na kuendeleza familia zetu kwa kupata lishe bora kupitia fursa mbalimbali zinazowalenga wanawake”. Amesema Ofisa huyo.

Pamoja na hayo, Materu pia ameeleza kuwa wanawake ni nguzo muhimu katika jamii huku akikemea vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto wa kike.

“Tusikubali kudhalilishwa, tuanze sisi wenyewe kukemea vitendo vya ukatili vinavyodhalilisha utu wa mwanamke, pia tuwafichue wanaowapa mimba watoto wetu wa kike wakiwa na umri mdogo na kuwakatisha masomo ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano kwa serikali ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya watu hao”. Amesisitiza Materu.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter