MKURUGENZI wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake( TAMWA- Zanzibar) Dkt.Mzuri Issa amewashauri wanawake wajasiriamali kisiwani Pemba kutumia vizuri neema ya zao la Karafuu kisiwani humo kwa kuzalisha bidhaa mbali mbali.
Dkt Mzuri aliyasema hayo leo Juni 27,2020 wakati alipokua akitizama baadhi ya bidhaa
zinazozalishwa na wajasirimaali hao kutoka Pemba huko ofisini kwake
Tunguu Wilaya ya kati Unguja.
Amesema zao la karafuu linaweza kuzalisha bidhaa mbali mbali ambazo
zinasoko kubwa ndani na je ya Nchi iwapo wajasiriamali hao wataweza
kuzisanifu vyema karafuu hizo.
Akitolea mfano wa bidhaa zinazotokana na karafuu alisema ni sabuni
pamoja na liwa ambalo ni maalumu na hutumika kwa ajili ya kusafishia
mwili kwa wanawake na wanaume(singo)
Pia Dkt, Mzuri aliwataka wajasiriamali hao kuanza kuangaza zaidi soko la
kimataifa ambapo pia kuna uhitaji mkubwa wa bidhaa za asili kutoka
Zanzibar hususani zinazoalishwa kwa kutumia karafuu na mengineyo.
Kwa upande wake afisa uwezeshaji wanawake TAMWA ofisi ya Pemba Asha
Mussa alisema wanawake wengi kisiwa cha Pemba wamehamasika na kujiunga kwenye vikundi mbali mbali vya uzalishaji wa bidhaa.
Akitolea mfano alisema pia wajasiriamali hao hawakuridhika tu na
uzalishaji wa bidhaa hizo pia wameanza kujiungiza katika ufuagaji ambapo
tayari baadhi ya vikundi vinamiliki mabanda ya na wanaendelea na ufugaji
kuku.
Akizungumzia kuhusu changamoto alisema bado zipo changamoto mbali mbali ikiwemo ukosefu wa soko la uhakika kwa wajasiriamali ambapo wakati mwengine wajasirimali hao hulazimika kukaa na bidhaa zao ndani kwa muda mrefu.
Afisa huyo uwezeshaji wanawake kiunchumi aliomba Serikali na taasisi
nyengine mbali ndani ya Zanzibar na nje ya Tanzania kujitokeza kwa wingi
kuunga mkono jitihada za vikundi hivyo kwa kuwa kufanya hivyo
kutawawezesha wanawake wengi kujikwamua kiuchumi na kuondokana na
umasikini.
Akizungumzia kuhusu hali halisi ya uzalishaji wa bidhaa mmoja miongoni
mwa wajasiriamali kutoka kisiwani Pemba Sakina Ame Bakar alisema
wanajitahidi katika uzalishaji wa bidhaa bora na zenye viwango vya hali
ya juu.
Alisema licha ya jitihada hizo lakini wanaendelea kukabiliwa na changamoto ya ukosefu wa soko bora na lenye uhakika kwao ambalo lingewafanya kwa wajasiriamali bora na wakimataifa.
Aidha ameiomba Serikali kuendelea kuwatengezea mazingira ikiwemo
kuwakutanisha na makampuni makubwa pamoja na wajasiamali wengine wa kimataifa ili waweze kutengeza masoko mapya.