Home FEDHA Serikali yatoa bilioni moja kutatua tatizo la maji

Serikali yatoa bilioni moja kutatua tatizo la maji

0 comment 91 views
Na Mwandishi wetu

Akiwa katika ziara ya kukagua uboreshaji wa huduma ya afya kwenye ngazi za zahanati na vituo vya afya, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Hamis Kigwangala amesema serikali imetoa zaidi ya shilingi bilioni moja katika Wilaya ya Longido ili wananchi wapate maji ya uhakika.

Kingwagala amesema serikali tayari imetoa fedha hizo kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo mkubwa wa maji ambao utamaliza kabisa tatizo la maji ambalo ni kero namba moja katika wilaya hiyo. Amewahakikishia wananchi katika wilaya hiyo kuwa makandarasi wanne wapo njiani kutekeleza mradi huo muda wowote kuanzia sasa.

Naibu Waziri huyo pia amewaambia wananchi katika wilaya ya Longido kuwa serikali ya awamu ya tano itatekeleza ahadi zake zote ikiwemo hiyo ya maji, hali ambayo itapelekea wananchi hao kutumia muda mwingi kufanya shughuli za maendeleo badala ya kutafuta maji.

Amewaonya wanasiasa wanaopotosha umma na kusema waiache serikali itekeleze miradi mbalimbali kwa ajili ya maendeleo ya wananchi wote kwani kwenye maendeleo hakuna siasa. Ameongeza kuwa serikali imejipanga kutatua kero za muda mrefu za wananchi wake.

Tags:

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter