Home KILIMO Wakulima wa Mihogo wapatiwa mafunzo Mkuranga

Wakulima wa Mihogo wapatiwa mafunzo Mkuranga

0 comment 140 views
Na Mwandishi wetu

Halmashauri ya Mkuranga mkoani Pwani na taasisi ya Cassava Adding Value for Africa (CAVA) zashirikiana kutoa mafunzo ya siku mbili kwa wakulima takribani 64 wa mihogo yaliyolenga kuokoa bidhaa zinazotokana na unga wa mihogo. Meneja wa mradi huo, Grace Mahende amesema lengo kubwa katika mafunzo hayo ni wajasiriamali kuongeza kipato chao ili wapatiwe masoko zaidi ya mihogo mibichi na mikavu.

Grace ameshauri wakulima kutumia unga bora wa mihogo na kuzingatia kuwa sio kila unga unatoa bidhaa ya hali ya juu. Pia ameshauri wakulima hao kutumia mashine za kusindika unga huo na kuachana na unga wa makopa. Wajasiriamali nao wametakiwa kutumia fursa kama hizi kujiongezea kipato na kufungua masoko.

Wakulima walioshiriki katika mafunzo hayo wamesema wamenufaika na elimu waliyoipata na itawawezesha wao kufanya kilimo hicho katika viwango vya juu zaidi na kutumia mbinu bora za uhifadhi.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter