Home FEDHA Halmashauri Dar yaendelea kuvutana na NSSF

Halmashauri Dar yaendelea kuvutana na NSSF

0 comment 33 views
Na Mwandishi wetu

Mgogoro unaoendelea kati ya Halmashauri ya jiji la Dar es salaam na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umechukua sura mpya baada ya Halmashauri ya jiji kuomba Waziri wa Fedha, Dk. Philip Mpango na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi George Simbachawene kuingilia kati mgogoro huo.

Mvutano huu umetokana na madai ya jengo la Machinga Complex ambalo NSSF walijenga kwa mkopo wa gharama ya Sh. 12.4 bilioni, lakini halmashauri wametakiwa kulipa kiasi cha Sh. 42 bilioni hivyo mfuko huo kupata faida yaSh. 30 bilioni kutokana na riba, fedha ambayo halmashauri hiyo imedai haina uwezo wa kulipa.

Akizungumzia juu ya suala hili, Meya wa jiji la Dar es salaam Isaya Mwita amesema tangu kumalizika kwa jengo hilo, deni limekuwa kwa kasi hivyo kupeleka wao kushindwa kulipa. Ameongeza kuwa jengo la Machinga Complex lina mapungufu mbalimbali hali inayopelekea Halmashauri hiyo kukusanya kodi isiyozidi milioni 500 kwa mwaka.

Mwita ameongezea kuwa wanataka kufanya mazungumzo na NSSF ili kufika suluhu  na ikishindikana, NSSF warudishiwe jengo hilo na kuliendesha kwa faida hadi deni hilo litakapomalizika. Amewataka wafanyabiashara kuendelea na shughuli zao kama kawaida hadi pale makubaliano yatakapofikiwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter