Home BIASHARAUWEKEZAJI Wawekezaji nchini watakiwa kutunza mazingira

Wawekezaji nchini watakiwa kutunza mazingira

0 comment 100 views
Na Mwandishi wetu

Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Dk. Reginald Mengi ameshauri wawekezaji hapa nchini kuzingatia hifadhi ya mazingira. Katika taarifa hiyo iliyosomwa kwa niaba yake na Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Godfrey Simbeye, Dk. Mengi amesema bila hewa safi, maji ya uhakika, maliasili na usalama, uchumi wa nchi hauwezi kukua.

Hayo yote yamesemwa katika mkutano wa kwanza wa mwaka wa Chama cha Wataalamu  wa Mazingira Tanzania (TEEA), ambao ulifanyika sambamba na uzinduzi wa katiba ya chama hicho. Dk. Mengi amesema katika taarifa yake kuwa chama hicho kimekuja kipindi muafaka kwani wataalamu hao wa mazingira watachochea mabadiliko ya uchumi na viwanda kwa kiasi kikubwa.

Ili kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda ni muhimu wadau wote ikiwemo wananchi na wafanyabiashara kushiriki ili kuleta maendeleo. Dk. Mengi pia ametoa wito kwa chama hicho kufanya kazi na serikali ili kusudi elimu ya kulinda mazingira kwa wananchi ikuzwe, huku akiongeza kuwa wawekezaji wa hapa nchini sasa watakuwa na maadili ya biashara yenye kulinda na kutunza mazingira.

Naye Mwenyekiti wa TEEA, Prof. Raphael Mwalyosi amesema ni jukumu la chama hicho kuhakikisha kuwa miradi yote ya maendeleo hapa nchini inaenda vizuri.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter