• Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
Wednesday, June 29, 2022
  • Login
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI
No Result
View All Result
Pesatu
No Result
View All Result

TARI YACHAGUA KITUO CHA UENEZAJI TEKNOLOJIA

Ni viwanja vya NANE NANE Mkoani SIMIYU

Jensen Kato by Jensen Kato
June 17, 2020
in KILIMO
0
Share on FacebookShare on Twitter

Kituo cha utafiti wa kilimo nchini (TARI) kimechagua eneo la viwanja vya maonesho ya nane nane vilivyopo  kata ya  Nyakabindi wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu kuwa kituo endelevu cha uenezaji wa teknolojia lengo likiwa kuwawezesha  wakulima kupata  huduma za kilimo kwa mwaka mzima.

Hayo yamebainishwa na Bibi. Mshaghuley Ishika kutoka TARI Dodoma kwenye kikao cha maandalizi nane nane kilichofanyika Juni 15, 2020 kwenye jengo la mkoa wa Simiyu lililopo kwenye viwanja hivyo kikwahusiaha viongozi wa Kanda ya ziwa Mashariki (Simiyu, Mara na Shinyanga).

Aidha, Ishika amesema kituo hicho kitawarahisishia wakulima kupata bidhaa zinazozalishwa kwenye Kituo hicho ambapo kwa hapa nchini huzalishwa katika vituo 17,  huku akibainisha kuwa TARI kwa kutambua hilo wameamua kuongeza eneo la vipando katika Viwanja vya Nyakabindi na kufikia hekari 3.

“Mbali na kuwa kituo endelevu cha usambazaji teknolojia kutakuwa vifaa na duka la mbegu zinazozalishwa na TARI  ambazo zinapatikana katika vituo 17 hapa nchini na  litamsaidia mkulima kujifunza mengi kuhusiana na kilimo; kituo hiki pia kimepatiwa mtumishi wa kudumu atakayekuwa anasambaza teknolojia kanda ya ziwa Mashariki ,” amesema Ishika.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Bw. Jumanne Sagini  amesema maandalizi ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa mwaka 2020  yamefikia 70% na kuongeza kuwa kwa upande wa vipando vimefikia 75%.

Wakati huo huo  Sagini amewaomba  viongozi wote wanaotoka  kwenye mikoa inayounda kanda ya ziwa Mashariki (Simiyu, Mara na Shinyanga) wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji  kuhudhuria kikamilifu kwenye vikao vya maandalizi ili yale wanayokubaliana wayatekeleze kwa wakati.

ADVERTISEMENT

Akizungumzia masuala  ambayo bado yanafanyiwa kazi Sagini amesema kwa sasa kamati ya maandalizi inaendelea na  ni ukarabati wa miundombinu ikiwemo   maji ,barabara na umeme huku akiwaomba washiriki kutoa michango yao mapema ili kufanikisha maandalizi kwa wakati.

Awali akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Mara,Mhe.Adam Malima, Mkuu  wa wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri ambaye pia  alikuwa Mwenyekiti wa kikao hicho, ameuhakikishia umma kuwa Maonesho ya Nanenane mwaka 2020 yatakuwa bora zaidi  na yataacha alama; kutokana na maonesho hayo  kufanyika kitaifa kwa miaka mitatu  mfululizo katika kanda ya ziwa Mashariki.

Katika hatua nyingine mhandisi Msafiri  amezitaka halmashauri zote ambazo hazijaanza na zile  ambazo maandalizi yake yanaenda taratibu, kuharakisha kusimamia maandalizi hayo na kuhakikisha yanakuwa ya kuridhisha, ili wakulima watakapokwenda kujifunza waone umuhimu wa kilimo chenye tija.

Kanda ya ziwa Mashariki inaundwa na mikoa mitatu ambayo ni Mara, Shinyanga na Simiyu na  mwenyeji wa maonesho ya Nane nane kitaifa ni mkoa wa Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo sasa, ambapo  kwa mwaka 2020 kaulimbiu ya maonesho haya ni “KWA MAENDELEO YA KILIMO MIFUGO NA UVUVI CHAGUA VIONGOZI BORA 2020”.

Jensen Kato

Jensen Kato

Next Post

SABABU ZA BIASHARA NYINGI KUKOSA WATEJA.

Discussion about this post

Habari Mpya

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

June 28, 2022

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

June 28, 2022

Mapendekezo bima ya afya kwa wote

June 28, 2022

Turkish Airlines yarejesha safari zake KIA

June 28, 2022
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amos Makalla akizungumza katika warsha ya viongozi wa Serikali wa mkoa na Bank ya NMB.

Benki ya NMB yapongezwa

June 28, 2022

Rais Samia azindua taasisi Zanzibar

June 28, 2022

KUHUSU SISI

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905. PesaTu inamlenga kila mtu ambaye kwa namna moja au nyingine anaguswa na anapenda kujua/ kufuatilia masuala mbalimbali ya kiuchumi ya nchi ikiwemo ujasiriamali, uwekezaji, viwanda, kilimo na hisa.

LATEST

Kilimo biashara, sekta yenye fursa za uwekezaji

by Jensen Kato
June 28, 2022
0

Kilimo biashara kinaendelea kukua barani Afrika na muda umefika kwa watu hususani vijana kuchagamkia fursa mbalimbali zinazotokana na kilimo. Watu...

Miamala ya simu yaongeza Pato la Taifa

by Pesatu Reporter
June 28, 2022
0

Miamala ya fedha kwa njia ya simu imechangia kuongezeka kwa pato la Taifa kutoka asilimia 40 mwaka 2013 hadi kufikia...

RECOMMENDED

Waziri Mwijange aja na orodha ya viwanda visivyofanya kazi

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

  Na Mwandishi wetu. Baada ya Rais John Magufuli kuonyesha kukerwa na kitendo cha Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji...

Nane Nane itumike kama darasa huru kwa wakulima

by Patricia Richard
March 23, 2018
0

Na Mwandishi wetu Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imejitolea kuwapa mafunzo ya siku moja wakulima mkoani Lindi...

No Result
View All Result
  • Home
  • FEDHA
    • MIKOPO
    • BIMA
    • HISA
  • BENKI
  • BIASHARA
    • UJASIRIAMALI
    • UWEKEZAJI
    • BIASHARA NDOGO NDOGO
  • VIWANDA
    • MIUNDOMBINU
    • NISHATI
    • UZALISHAJI
  • KILIMO
    • KILIMO BIASHARA
    • KILIMO UFUNDI
  • MAHOJIANO
  • AFRIKA MASHARIKI
    • BIASHARA
    • FEDHA
    • UJASIRIAMALI

© 2022 JNews - Premium WordPress news & magazine theme by Jegtheme.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In