Home KILIMO Wakulima washauriwa kuzalisha mpunga kwa wingi zaidi

Wakulima washauriwa kuzalisha mpunga kwa wingi zaidi

0 comment 221 views
Na Mwandishi wetu

Japo kuwa Tanzania inasifika kwa uzalishaji wa mpunga, imeelezwa kuwa uzalishaji huo haujitoshelezi kusaidia nchi nyingine barani Afrika ambazo hutumia dola za kimarekani takribani bilioni 5 ili kuagiza mchele kutoka mabara mengine ambapo kiasi hicho cha fedha hununua tani milioni 14,000 za mchele.

Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa shirika la kimataifa la African Rice kwa nchi za kaskazini na kusini mwa Afrika, Josey Kamanda katika warsha ya kilimo bora cha mpunga ambayo inaendelea mkoani Morogoro. Amesema kuna haja ya kuwasukuma zaidi wakulima juu ya kuzalisha zaidi zao hilo. Ameongeza kuwa upungufu wa mchele barani Afrika unatokana na ukosefu wa nyenzo za kutosha ili kulima zao hili hivyo ni muhimu kuongeza maeneo mengi ili kusudi uzalishaji nao uongezeke.

Kamanda pia amesisitiza kuwa African Rice ina jukumu la kusaidia wakulima ili kukuza na kupata mazao mengi ya mpunga hivyo wakulima kujiongezea kipato na uchumi wa nchi kwa ujumla. Naye Mkuu wa wilaya ya Kilombero Bw. Lephy Gembe amesema wilaya yake inaendelea kuboresha mabonde na mito iliyopo ili kuongeza uzalishaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter