Home Elimu FUGA SAMAKI KISASA

FUGA SAMAKI KISASA

0 comment 139 views

Endapo watanzania watabadilika na kutumia mbinu za kisasa za kilimo na ufugaji ikiwemo ufugaji wa samaki basi wanaweza kujiingizia kipato na kupiga hatua kimaisha. Ufugaji  huu ni nafasi nzuri kwa wadau kufanya kilimo mseto na kutumia ardhi kwa mazao na mifugo hivyo kupata faida zaidi.

Ufugaji huu unachohitaji zaidi ni ardhi ya kutengezea bwawa. Upatikanaji wa maji ya uhakika pia ni jambo la msingi. Kwa mfugaji mdogo mbinu nyingine za kuhifadhi maji kama kutumia debe inaweza kutumika. Ufugaji huu unahitaji umakini mkubwa hivyo inashauriwa mfugaji kuwa na ufahamu kuhusiana na samaki. Muda gani wa kuwalisha, usafi wa bwawa na kipimo ambacho maji yanatakiwa kuwepo muda wote.

Baada ya hili kukamilika mfugaji anaweza kuamua ni aina gani ya samaki anataka. Zipo aina mbalimbali za samaki ambao wanaweza kufugwa nyumbani. Sato na Kambale ndio wanaofugwa kwa wingi. Hakikisha kuwa kila mita moja ya mraba samaki hawazidi 8. Si vizuri kuwajaza wengi katika eneo dogo kwani watakosa hewa.

Ni muhimu kuwa makini wakati wa kununua vifaranga vya samaki. Ni vizuri kujiridhisha kuwa mbegu unazonunua zipo katika hali nzuri. Mbegu ya sato hupatikana kwa bei ya rejareja kuanzia 300 Sh huku kambale ikiwa ni 500 Sh kwa kifaranga kimoja. Tanzania Fisheries Research Institute (TAFIRI) ya Nyegezi Mwanza ni moja kati ya sehemu ambazo vifaranga hivi hupatikana.

Kwenye chakula, samaki hula kulingana na uzito wao. Wakiwa wadogo wanakula asilimia 5 ya uzito wao na kadri wanavyoongezeka hufikia hadi asilimia 3. Ni muhimu kufahamu kuwa kuna aina mbili za chakula cha samaki.

Cha kwanza ni chakula cha asili kinachotokana na mbolea ambacho huchanganywa na maji na kukaa kwa angalau siku 21. Kufanya hivi kunawatengenezea samaki mazingira mazuri ya kujitafutia chakula chao wenyewe. Mara nyingi kinakuwa katika mfumo wa mimea au vijidudu.

Aina ya pili ni chakula ambacho mfugaji hupaswa kuwalisha samaki. Ni muhimu kuwa na muda maalum wa kuwapatia chakula ambao haubadiliki mara kwa mara ili kujenga mazoea na kuwa na rekodi ya muda gani samaki wanakula.

ADVERTISEMENT

Wafugaji wa samaki wana haja ya kuwa watunzaji na wachukuaji takwimu. Rekodi za uzalishaji na mauzo yao zitasaidia kwenye uombaji wa mikopo kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za kiserikali. Ufugaji huu unaashiria matumaini makubwa. Tukiendelea hivi, hata serikali nayo itasukumwa kuweka nguvu nyingi zaidi katika sekta hii ya ufugaji wa kisasa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter