Home Elimu Kikwete aitaka UDSM kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wahitimu

Kikwete aitaka UDSM kutatua changamoto ya ukosefu wa ajira kwa wahitimu

0 comment 107 views

Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kimezindua programu ya kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu ili kuweza kukidhi vigezo katika soko la ajira kwa kushirikiana na Taasisi ya Gen Empower ambapo Rais mstaafu ambae pia ni Mkuu wa chuo hicho, Dkt. Jakaya Kikwete alisema ana imani itakuwa chanzo cha kuondoa na kumaliza kabisa tatizo la ajira nchini.

“Isiwe fahari kwa wanafunzi kukaa vyuoni kwa miaka mitatu au zaidi na kuishia kuvaa majoho na kurejea majumbani,” amesema Dkt. Kikwete katika uzinduzi programu ya kuwajengea uwezo wanafunzi wanaohitimu elimu ya juu ili kuweza kukidhi vigezo katika soko la ajira.

Programu hiyo ya miaka mitano, imelenga kuwaongezea vijana ujuzi na maarifa ili kuweza kupata ajira na kujiari wenyewe badala ya kusubiria ajira.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter