Benki ya CRDB imeshinda tuzo ya Benki Bora ya Uwasilishaji wa hesabu za fedha kwa mwaka 2018/2019.
Tuzo hiyo imetolewa na Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi kwa kuitambua Benki ya CRDB kama benki bora katika uwasilishaji wa hesabu za fedha.
Taarifa kutoka benki hiyo inasema “tunafurahi kuibuka washindi wa kwanza wa tuzo ya uwasilishaji bora wa taarifa za fedha 2019 kutoka Bodi ya Taifa ya Uhasibu (NBAA) katika kipengele cha mabenki. Kuwajibika kwetu katika misingi ya utawala bora ndio siri ya ushindi wetu”.
Siku chache zilizopita, Benki hiyo ilitambuliwa kuwa benki bora nchini na Taasisi ya Kimataifa ya Global Finance.