Home BIASHARA Rais Mwinyi akaribisha wawekezaji wa Kenya

Rais Mwinyi akaribisha wawekezaji wa Kenya

0 comment 124 views

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi amewakaribisha wafanya biashara nchini kwenya kuja kuwekeza Zanzibar.

Akifanya mazungumzo na Gavana wa Mombasa nchini Kenya, Ali Hassan Joho, rais Mwinyi amesema pande hizo mbili zina historia katika seka ya biashara.

Dk Mwinyi amemweleza Gavana Joho kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na wafanyabiashara wenye lengo la kuwekeza na kufanya biashara visiwani humo.

Rais Mwinyi amesema SMZ imeweka mikakati maalumu katika kuwavutia wawekezaji kwa kupitia Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) itaendelea kuweka mazingira bora.

Gavana Joho ambae amefatana na ujumbe wa baadhi ya wafanyabiashara kutoka Mombasa amemweleza rais Mwinyi kuwa wafanyabiashara hao wapo tayari kufanya biashara kati ya pande hizo mbili na baadhi wameshaanza mchakato wa biashara.

Amesema historia inaonesha Zanzibar na Mombasa zina uhusiano na ushirikiano wa miaka mingi hivyo ni vyema ukaimarishwa.

Ameeleza kuwa upande wa utalii ambayo mazingira yake kwa pande hizo mbili hushabihiana, ni vyema paepo ushirikiano ili wazidi kupanua wigo na kuikuza sekta hiyo kwa manufaa ya pande zote mbili.

Wafanyabiashara hao wamesema wanaamini soko la Zanzibar litawasaidia kwa kiasi kikubwa kwani wataweza kuuza bidhaa zao karibu tofauti na sasa ambapo wanauza katika nchi zilizombali na Mombasa kama vile Congo, Zambia na Burundi.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter