Home BIASHARA Bei ya vifurushi kurejea kama zamani

Bei ya vifurushi kurejea kama zamani

0 comment 302 views

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imesema wanafuatilia kwa karibu sana na kwa kushirikiana na watoa huduma za mawasiliano nchini kuhakikisha kuwa suala la vifurushi vya simu linarejea kama ilivyokuwa hapo awali.

Akizunguza Dar es Salaam leo Jumatano Aprili 14, 2021, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Dk. Jabir Bakari amesema “kama ambavyo maelekezo ya serikali yanavyosema, tunafuatilia kwa karibu sana kuhakikisha kwamba vifurushi vinarudi katika hali yake ya kawaida kama ilivyokuwa hapo awali.”

Amesema wanategemea mabadiliko hayo kufanyika ndani ya siku mbili au tatu na  maelekezo ni kwamba vifurushi vyote vitarudishwa kama ilivyokuwa.

Ameeleza kuwa “kilichotokea ni kwamba kampuni za simu zilikuwa zinatumia maelekezo mapya jambo ambalo limeleta changamoto, lakini sasa hivi tunarejesha huduma zote kama awali,” amesema Dk. Bakari.

Aidha, Dk. Bakari amesema kuwa sababu ya kubadilisha vifurushi hivyo awali ilikuwa ni kutokaa na kuwapo kwa wingi wa vifurushi hatua ambayo ilikuwa ikiwachanganya baadhi ya watuamiaji.

Nae mtumia wa simu ya mkononi mkazi wa Dar es Salaam aliejitambulisha kwa jina la Richard amesema bando zirudi kama zamani ikiwezekana hata gharama zipungue kwa kuwa wanaoumia ni watumiaji hususani ambao wanafanya biashara zao kwa njia ya mtandao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter