Home KILIMO Ukosefu wa mitaji, riba kubwa kikwazo kwa wakulima wadogo

Ukosefu wa mitaji, riba kubwa kikwazo kwa wakulima wadogo

0 comment 188 views

Ukosefu wa upatikanaji wa mitaji na riba kubwa zinazotozwa na taasisi za kifedha umetajwa kuwa sababu kubwa inayowakwamisha wakulima wadogo  kufanya kilimo cha kisasa Tanzania.

Loveness Adolf, ni Afisa Uhusiano wa asasi ya kilele ya sekta binafsi ijulikanayo kwa jina la TAHA ambayo inatetea ukuaji na ushindani wa kilimo cha mbogamboga nchini amesema hali hiyo inapelekea wakulima wengi kushindwa kuzalisha kwa viwango vinavyohitajika kwenye soko.

Adolf amebainisha hayo katika Maonyesho ya 45 ya Biashara ya Kimataifa  jijini Dar es Salaam (sabasaba).

“Mahitaji ya mazao sokoni ni makubwa, lakini uzalishaji bado ni mdogo na haukithi viwango vya soko, hii ni kutokana na wakulima wengi wadogo kushindwa kulima kisasa kutokana na kukosa mitaji na kumudu gharama za riba.” amesema Adolf.

“Tunashirikiana na serikali na wadau mbalimbali wa maendeleo katika kutatua changamoto zinazokwamisha maendeleo ya tasnia hii nchini, pia tunaunganisha wakulima na taasisi za kifedha kwa mikopo na misaada ya kifedha ya bei nafuu. lakini bado kuna changamoto katika upatikanaji wa mitaji” amesema.

Amesema TAHA ambayo ilianzishwa mwaka 2004, ina wanachama 43,000 ikijumuisha wakulima wakubwa, watoa huduma na wakulima wadogo ambapo wakulima wadogo ni takribani asilimia 60 ya wanachama wote.

Akielezea jinsi ya kuwa mwanachama wa TAHA amesema mkulima apaswa kulima kuanzia robo eka na huku akiwa na chanzo cha kuaminika cha maji kwa ajili ya umwagiliaji.

“Mkulima atapatiwa ujuzi wa kulima kisasa, kupewa bwana shamba wa kumuelimisha na kufuatilia kila hatua mpaka mazao yanapovunwa, pia huwa tunawaunganisha wakulima na wanunuzi wa mazao yao.” Amesema

“Tumelenga sana makundi ya wanawak na vijana, lakini kw aupande wa wanawak kuna changamoto katika suala la umilikii wa ardhi hususani mikoa ya kanda ya ziwa” amesema.

Ameeleza kuwa huwa wanawafikia wanachama wao pamoja na wakulima kupia serikali za mitaa ambapo wawakilishi wao hufika huko pamoja na kupitia mikutano mbalimbali na maonyesho.

Ameleza kuwa, tangu kuanzishwa kwake mwaka 2004, TAHA imekuwa jukwaa la kutoa sauti kwa wazalishaji, wafanyabiashara, wauza bidhaa nje na wasindikaji wa mazao ya mbogamboga, matunda, mimea tiba, viungo, mazao yatokanayo na mizizi pamoja na maua.

TAHA inaendesha kazi zake katika amikoa 25 Tanzania Bara na Visiwani. Mikoa hiyo ni pamoja na Arusha, Mwanza, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Dodoma , Morogoro, Iringa, Njombe, Mbeya, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Mara, Simiyu, Shinyanga, Singida, Songwe, Unguja na Pemba.

 

 

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter