Benki ya CRDB imetangaza punguzo la riba za mikopo ya kilimo na wafanyakazi.
Taarifa ya CRBD inasema riba ya mikopo ya kilimo imepunguzwa kutoka 20% hadi 9%, huku ya wafanyakazi ikiwa ni 13% kutoka 16%.
CRDB imetangaza punguzo hilo leo January 24, 2022 na kusema punguzo hilo limelenga kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Ikumbukwe kuwa, riba kubwa inayotozwa na taasisi za fedha imekuwa ikitajwa kama moja ya changamoto kwa wananchi wenye kipato cha chini kushindwa kumudu mikopo.
Mwishoni mwa mwaka jana, mbunge wa Vunjo Dk Charles Kimei alisema Bungeni Dodoma kuwa uwepo wa riba kubwa imekuwa ni faida kubwa ya benki na wanahisani wake lakini kwa wananchi ni maumivu.
Dr Charles Kimei, ambae amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB alisema riba ikishuka itasaidia wananchi wengi kukopa kwa wingi na kufanya taasisi za fedha kuwa rafiki na wafanyabiashara.
“Riba ya asilimia 15 ni mateso kwao na ilipaswa jambo hilo lipitiwe na kutazamwa upya ili kuishusha kwa kuwa duniani kote sera ya fedha ni riba sio kingine’ alinukuliwa Dr Kimei.
Alieleza kuwa Sera ya fedha Tanzania bado ina upungufu mkubwa kwa kuwa haigusi watu wenye kipato cha chini.
Soma: Vijana na kilimo biashara