Home BIASHARAUWEKEZAJI Rais Samia aenda Ghana

Rais Samia aenda Ghana

0 comment 136 views
Rais Samia Suluhu Hassan anaondoka nchini leo kuelekea Accra, Ghana kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku tatu.
Akiwa nchini Ghana, Rais Samia anatarajia kushiriki mdahalo wa Wakuu wa Nchi utakaojadili fursa zilizomo na changamoto zinazozikabili nchi za Afrika ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabia nchi, kupanda kwa bei ya vyakula na matumizi ya nishati endelevu.
Rais Samia pia anatarajia kupokea Tuzo ya mwaka 2022 ya Babacar Ndiaye kwa mafanikio ya serikali ya awamu ya sita katika ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ambayo hutolewa kwa Mkuu wa Nchi iliyofanya vizuri zaidi.
Tuzo hiyo hutolewa kila mwaka katika Mkutano wa AfDB, ambao kwa mwaka 2022 unafanyika Accra, Ghana.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter