Home FEDHAMIKOPO Epukeni kukopa kwa wasio na leseni: BoT

Epukeni kukopa kwa wasio na leseni: BoT

0 comment 118 views

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewataka wananchi kuepuka kukopa au kufanya biashara na taasisi, kampuni au mtu/watu binafsi ambao hawana leseni.
Taarifa ya BoT iliyotolewa Novemba 24, 2022 inasema “imebaini kuna baadhi ya taasisi, kampuni na watu binafsi wanaojihusisha na biashara ya kutoa mikopo bila ya kuwa na leseni, jambo ambalo ni kinyume na Kifungu cha 16(1) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018.
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuutaarifu umma kuwa taasisi, kampuni na mtu binafsi wasio na leseni husika hawaruhusiwi kufanya biashara ya kukopesha.”

Taarifa hiyo ya Gavana wa BoT imefafanua kuwa “kwa mujibu wa Kifungu cha 16(2)(a) cha Sheria ya Huduma Ndogo za Fedha ya mwaka 2018, hatua zitakazochukuliwa kwa ukiukaji wa Sheria hiyo ni pamoja na faini isiyopungua Sh20 milioni au kifungo kwa muda usiopungua miaka miwili.

Leave a Comment

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter