Home VIWANDAUZALISHAJI Meli ya Coral Geographer Tanzania

Meli ya Coral Geographer Tanzania

0 comment 100 views

Meli ya kifahari ya watalii ijulikanayo kwa jina la “Coral Geographer” imetia nanga kwa mara ya kwanza Machi 7, 2023, katika Pwani ya Afrika Mashariki hususani katika fukwe za mji wa kihistoria wa Kilwa.

Meli hiyo iliyobeba watalii 120 kutoka nchini Australia pia inakwenda visiwa vya Karafuu Zanzibar.

Meli hiyo yenye hadhi ya nyota tano, imeleta watalii ambao wametembelea Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni ya Magofu ya Kale, Kilwa Kisiwani na Songo Mnara na kufanya utalii wa malikale pamoja na utalii wa fukwe.

Tangu Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ashiriki filamu ya Royal Tour idadi ya watalii wanaokuja nchini imekuwa ikiongezeka maradufu.

Mwenyekiti Mwenza na Mmiliki wa kampuni ya kitalii ya Abercrombie and Kent iliyoratibu ziara hiyo, Manfredi Lefebvre ni miongoni mwa watu mashuhuri ambao Rais Samia alikutana nao jijini New York wakati wa uzinduzi wa filamu ya Royal Tour April mwaka jana na kumshawishi kushirikiana na Tanzania.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter