Home BIASHARA Watanzania watakiwa kuchangamkia  fursa soko la Malawi

Watanzania watakiwa kuchangamkia  fursa soko la Malawi

0 comment 126 views

Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (TanTrade) 9Machi 2023 imeratibu mkutano Kwa njia ya Teknolojia ya Mtandao baina kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Malawi wenye lengo la kujadili fursa za kibiashara zilizopo kati ya Tanzania na nchi ya Malawi.

Mkutano huo umeshirikisha Taasisi mbalimbali za serikali pamoja na Wafanyabiashara.

Akizungumza katika mkutano huo, Balozi wa Tanzania nchini Malawi Humphrey Polepole ameeleza kuwa nchini Malawi  kuna fursa mbalimbali zinazopatikana  katika sekta ya kilimo, ujenzi, mafuta , bidhaa za viwandani, chakula cha mifugo.

Ametaja pia uwepo wa kiwanda kikubwa cha mbao cha MDF ambacho kinazalisha mbao kwa wingi na kusambaza kwenye masoko mbalimbali.

Imeelezwa kubwa bidhaa zinazouzwa na Tanzania nchini Malawi ni pamoja na bidhaa za viwandani kama vile sabuni ya kufulia na usafi, bidhaa za urembo na vipodozi, bidhaa za glasi kama vile chupa na vifungashio, mifuko, nguo, vifaa vya shule na magari.

Kadhalika bidhaa zinazonunuliwa na Tanzania kutoka nchini Malawi ni pamoja na bidhaa za kilimo hususni karanga zenye maganda mekundu, maharage, soya na bidhaa za viwanda mathalani mashudu, sukari na mbao.

Pia Balozi polepole ametoa wito kwa wafanyabiashara kutoka Tanzania kushiriki kwa wingi katika kongamano la kibiashara litakalojulikana kama Tanzania-Malawi Trade and Investment Forum litalofanyika nchini Malawi Aprili 26 hadi 28 2023, lenye lengo la kushirikisha Wafanyabiashara wa sekta mbalimbali  kutoka Tanzania na Malawi na kuwapatia fursa za kupanua wigo wa biashara.


Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Latifa Mohamed Khamis amesema kuwa kikao hicho kina lengo  la kujadili fursa za ukuzaji na uendelezaji wa mahusiano ya biashara baina ya wafanyabiashara wa Tanzania na  Malawi.
“Katika miaka mitano iliyopita biashara ya bidhaa kati ya Tanzania na Malawi ilikuwa ni Dola za Marekani (USD) milioni 73.5 sawa na shilingi bilioni 171.4 , ambapo Tanzania ilikuwa na mauzo nchini Malawi ya USD milioni 52.8,” amebainisha.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter