Home KILIMO Walima kahawa wapewa mbinu kujikomboa kiuchumi

Walima kahawa wapewa mbinu kujikomboa kiuchumi

0 comment 100 views
Na Mwandishi wetu

Meneja wa Shirika lisilo la kiserikali la HRNS Webster Miyanda amesema wakulima wa zao la kahawa hapa nchini wataendelea kutokufanikiwa kiuchumi kama watazidi kuuza kahawa yao kwa walanguzi ambao wananunua kwa bei ya chini.

Miyanda amesema hayo kwa wakulima wa kata ya Nambinzo wilayani Mbozi mkoani Songwe alipokuwa anakabidhi mashine ya kukoboa kahawa inayogharimu zaidi ya Sh. 10 milioni.

Ameongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona wakulima wanatumia pesa, muda na nguvu nyingi kuzalisha zao hilo huku wanaonufaika ni watu kutoka nje ya Mbozi ambao wananunua kahawa hiyo kwa bei ya chini na kuwaacha wakulima hao katika umaskini.

Ameshauri wakulima hao kushirikiana na kuunda vikundi ambavyo vitakausha, kukoboa na kuuza kahawa mnadani kwa umoja ili kupata faida. Kwa upande wake,  Meneja wa Bodi ya Kahawa wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Zani Edmund amesema ili kahawa iwe na ubora unaotakiwa sokoni, ni vema wakulima waiandae kwa umoja. Amesisitiza pia juu ya uwepo wa vikundi ambavyo amedai vitasaidia wakulima kuongeza uzalishaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter