Home BENKI Madeni, mali Yetu Microfinance benki yahamishiwa NMB

Madeni, mali Yetu Microfinance benki yahamishiwa NMB

0 comment 104 views

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imehamisha mali na madeni ya Yetu Microfinance Bank Plc kwenda Benki ya NMB kuanzia Mei 24, 2023.

Hatua hiyo imekuja baada ya BoT kuiweka chini ya usimamizi Yetu Microfinance Bank Plc kwa ajili ya kupata ufumbuzi wa matatizo yanayoikabili ya mtaji na ukwasi mnamo Disemba 12, 2022.

Taarifa ya BoT inasema kwa kipindi hicho shughuli za biashara za Yetu Microfinance Bank zilisimamishwa kuiwezesha Benki Kuu kutathimini hatua stahiki za kuchukua.

“Benki Kuu ya Tanzania inapenda kuujulisha umma kuwa, kamujibu wa kifungu cha 59 (4)

cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006 mchakato wa kupata suluhisho la Yetu Microfinance Bank Plc umekamilika.

Uhamishaji wa mali na madeni kwenda benki nyingine ndio hatua stahiki iliyofikiwa,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo inasema kwa mujibu wa kifungu cha 58 (2) (h) cha Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha ya mwaka 2006, BoT imehamisha mali zote na madeni ya Yetu Microfinance Bank Plc kwenda benki ya NMB.

BoT imesema wenye amana na wadai wengine wa benki hiyo watapewa taarifa ya namna na siku watakayoanza kupata huduma za kibenki kupitia benki ya NMB.

Aidha, wateja wenye mikopo wanatakiwa kuendelea kulipa marejesho yao kwa mujibu wa mikataba yao ya mikopo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter