Home BENKI Vijana wenye biashara changa kunolewa

Vijana wenye biashara changa kunolewa

0 comment 77 views

Biashara changa za vijana 196 (startups) zimeingia katika hatua ya mafunzo kabla ya kupewa mitaji wezeshi kwa ajili ya kuendeleza biashara zao.

Taasisi ya CRDB Bank Foundation imezindua kambi ya mafunzo (boot camp) kwa ajili ya vijana hao.

Uzinduzi wa kambi hiyo umefanyika katika kituo maalum cha kuendeleza biashara changa kilichopo Makao Makuu ya zamani ya Benki ya CRDB jijini Dar es Salam na kuhudhuriwa na viongozi wa Benki, CRDB Bank Foundation, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), na Tume ya TEHAMA (ICTC).

Katika kambi hiyo biashara changa zitapewa mafunzo juu ya usimamizi wa uendeshaji, utawala bora, matumizi ya mifumo ya kidijitali, vihatarishi na udhibiti wa biashara, pamoja na fursa za uwekezaji katika masoko ya mitaji.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter