Home VIWANDAUZALISHAJI Serikali kutunga Sera ya kampuni changa za ubunifu

Serikali kutunga Sera ya kampuni changa za ubunifu

0 comment 102 views

Serikali imesema ina mpango wa kutunga Sera ya Kampuni Changa za Ubunifu (startups) ili kulinda kazi za ubunifu nchini.

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia Nape Nnauye amesema hayo Agosti 14, 2023 jijini Dar es Salaam.

“Sababu ya kuja hapa ni kwa sababu hii sekta inakuwa, takwimu zinaonesha kwamba kuna ongezeko kubwa sana la asilimia karibia 15 ukianzia mwaka jana.

Waziri Nape amebainisha kuwa “kwa takwimu zilizopo mwaka jana sekta hii imevutia uwekezaji wa utalii nchini wa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 80. Najua yapo mazao ambayo hata hayafiki nusu ya hiyo kwa iyo utaona ni jambo kubwa linavutia uwekezaji.”

Wabunifu wamekuwa wakibuni mambo mengi sana na mengine kutumika hadi nje ya mipaka yetu, baadhi ya vijana wetu wamefanya ubunifu, kwa sababu ya kukosekana kwa mifumo ya kisheria mizuri, imelazimika zile bunifu zao kutumiwa na nchi zingine na tunayo mifano,” ameeleza Nape.

Amesema ongezeko hilo limefanya Serikali ifungue macho zaidi kuona ni namna gani inaweza kusaidia vijana wabunifu ambao wanajiajiri na kuleta ufumbuzi wa mambo mbalimbali ambayo yataisaidia nchi.

Aidha, ameeleza kuwa mpango huo utashirikisha wadau wa pande zote mpaka kukamilika kwake ili kuweza kuwa na Sera Bora ya kusimamia kampuni hizo.

“Serikali inakamilisha hatua za mwanzo za utungwaji wa sera ya Startups na itakapokamilika italetwa kwenu wadau kwa ajili ya kutoa maoni yenu.” Amesema Waziri Nape

Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Startups Association (TSA), Zahoro Muhaji amesema kutokuwepo kwa sera hiyo kunawazuia kuweza kufanya biashara na wanafurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Serikali katika kukamilishwa kwa mchakato huo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter