Home KILIMO Kongamano la kilimo kukutanisha wadau 3000

Kongamano la kilimo kukutanisha wadau 3000

0 comment 170 views

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amewaalika Watanzania kushiriki katika kongamano la Kimataifa la Mifumo ya Chakula barani Afrika.

Kongamano hilo litawaleta pamoja wadau zaidi ya 3000 wa kilimo duniani ambapo kutakuwa na wawasilisha maada 350 kutoka nchi zaidi ya 70.

“ Mwaka huu taifa letu lilishiriki katika kinyang’anyiro kwa ajili ya kutaka kuaanda tukio kubwa la kilimo Afrika maarufu AGRF.

Niwakaribishe Watanzania wote katika tukio hilo la AGRF mwaka huu ambalo litawakutanisha na watu kutoka sehemu mbalimbali dunia na ni tukio muhimu sana katika sekta ya kilimo,” ameeleza Waziri Bashe.

Waziri Bashe ameeleza kuwa tukio hilo hufanyika mara moja kwa mwaka na hukutanisha watu mbalimbali duniani ikiwemo wadau wa sekta ya kilimo, maendeleo, watafiti, tasisis za fedha, viongozi mbalimbali ambao ni watunga sera na wakulima wakubwa.

“Mwaka huu Tanzania imepata heshima ya kuandaa tukio hilo ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alizindua tukio hilo mnamo mwanzoni mwa mwaka huu na kuitangazia dunia kuwa Tanzania imeshinda kuandaa Africa Food System Forum (AFSF),” ameeleza Bashe.

Amebainisha kuwa kongamano hilo linatarajia kufanyika Septemba 05 hadi 08 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter