Home WANAWAKE NA MAENDELEO Benki ya Wanawake yaipa sifa Tanzania

Benki ya Wanawake yaipa sifa Tanzania

0 comment 92 views

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluu Hassan

Na Mwandishi wetu

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema wakati akifungua tamasha la 14 la kijinsia ambalo limeandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) kuwa, Tanzania imepata sifa kubwa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (AU) aliohudhuria kupitia Benki ya Wanawake na jitihada zake mbalimbali za uwezeshaji wanawake kiuchumi.

Ameongeza kuwa serikali bado inaendelea kufanya michakato mbalimbali kama vile kuanzisha mifuko ya uwekezaji, vikoba na saccos ili kuwainua wanawake. Pia Makamu huyo wa Rais amesema serikali inalenga kuifufua benki ya wanawake ambayo kwa sasa inaonekana kulegelega ili isimame na kufanya kazi zake kwa malengo ambapo haitosaidia wanawake tu, bali hata wanaume watanufaika nayo.

Mbali na hayo, Samia ametoa agizo kwa Jeshi la Polisi kuchukua hatua dhidi ya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia katika jamii kwani vitendo hivi vimezidi kuongezeka hapa nchini. Ametaka Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Lazaro Mambosasa kuhakikisha vitendo hivyo vya ukatili vinakomeshwa hapa nchini.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter