Home VIWANDAUZALISHAJI Uvunaji wa samaki wapaa kwa asilimia 114.3 mbinga

Uvunaji wa samaki wapaa kwa asilimia 114.3 mbinga

0 comment 157 views

Uvunaji wa samaki katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga mkoani Ruvuma uliongezeka kwa asilimia 114.3 kwa mwaka wa fedha 2022/2023 ikilinganishwa na mwaka 2021/22.

Afisa uvuvi wa Halmashauri ya Mji wa Mbinga Musa Mwasenga amesema hayo Novemba 21, 2023, kuwa katika kipindi hicho uvunaji wa samaki uliongezeka kutoka tani 0.7 hadi kufikia tani 1.5.

“Ongezeko hilo limetokana na wafugaji wa samaki kuendelea kupata elimu kuhusu njia bora za ufugaji wa samaki,” amesema Mwasega.

Ameeleza kuwa “tumekuwa tukitumia Redio na semina mbalimbali kutoa elimu kwa wafugaji kuhusu ufugaji bora wa samaki. Pia tumekuwa tukimfikia mfugaji mmoja mmoja na ofisi zetu ziko wazi kwaajili ya ushauri.”

Mwasenga amesema katika Halmashauri hiyo ambayo hutegemea samaki kutoka kwenye mabwawa pekee, kuna wafugaji wa samaki 448.

Amebainisha kuwa, kati ya wafuhgaji hao 448, wafugaji 205 wapo kwenye vikundi na 243 ni mtu mmoja mmoja.

Kwa upande wa mabwawa ya kufugia samaki amesema yaliongezeka kutoka 529 mwaka 2021/22 hadi kufikia 594 mwaka 2022/23.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter