Home VIWANDAUZALISHAJI Tumeazimia kuifungua pemba kiuchumi: Rais Mwinyi

Tumeazimia kuifungua pemba kiuchumi: Rais Mwinyi

0 comment 82 views

Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameeleza kuwa Serikali imeazimia kuifungua Pemba kiuchumi kwa kutekeleza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Pemba, barabara za kutoka Chake hadi Mkoani, Chake hadi Wete, pamoja na bandari za Wete, Shumba Mjini, na Mkoani.

Dk. Mwinyi ameyasema hayo Agosti 21, 2024, wakati akizungumza na wajumbe wa Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu ya CCM ngazi ya Tawi, Wadi, Majimbo, Wilaya, na Mkoa katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha, Dk. Mwinyi amewahimiza wanachama wa CCM kuhubiri amani, umoja, na mshikamano. Pia alitumia fursa hiyo kuwahamasisha wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Kupiga Kura mwakani.

Rais Dk. Mwinyi amesema kuwa ametekeleza vema Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwa kuvuka malengo ya ilani hiyo katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, barabara, masoko, na kadhalika.

Halikadhalika, Dk. Mwinyi ameeleza kuwa CCM itashinda kwa kishindo mwaka 2025 kwa sababu imetekeleza vema ilani na kuvuka malengo waliyoyaahidi kwa wananchi.

Vilevile, Dk. Mwinyi amesema kuwa katika awamu mpya ya mwaka 2025-2030, kasi ya maendeleo ya Zanzibar itakuwa ya hali ya juu.

Kwa upande mwingine, Dk. Mwinyi amesema kuwa Serikali itamaliza changamoto za miradi ya umeme na maji katika kipindi kilichobaki, pamoja na kutekeleza ahadi zote zilizoahidiwa wakati wa kampeni za mwaka 2020.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter