Home VIWANDAMIUNDOMBINU TANROADS kuanza ujenzi daraja la Jangwani

TANROADS kuanza ujenzi daraja la Jangwani

0 comment 300 views

Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema Wizara kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) inatarajia kuanza kutekeleza mradi wa kimkakati wa Ujenzi wa Daraja la Jangwani.

Bashungwa ameesema hayo Mei 29,2024 bungeni jijini Dodoma wakati wa kuwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara na taasisi zake kwa mwaka 2024/2025.

Amesema mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa maendelezo ya Bonde la Mto Msimbazi.

Bashungwa amesema daraja hilo litakalojengwa lina urefu wa mita 390 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa mita 710 na kina cha mita 15.5 kutoka usawa wa bahari.

“Daraja hili litakapokamilika litatatua changamoto ya kujaa kwa maji katika barabara ya Morogoro eneo la Jangwani wakati wa mvua na kusababisha kufungwa kwa barabara hiyo mara kwa mara.”

Bashungwa amesema tathmini ya zabuni ili kumpata Mkandarasi na Mhandisi Mshauri zinaendelea.”

Jangwani ni mojawapo ya maeneo ambayo hukumbwa na mafuriko ambayo hupelekea barabara ya Morogoro kufungwa jambo ambalo huleta adha kwa watumiaji wa barabara hiyo.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter