Home Elimu Bilioni 32 zanufaisha miradi ya utafiti, ubunifu

Bilioni 32 zanufaisha miradi ya utafiti, ubunifu

0 comment 19 views

Serikali imesema kuanzia mwaka 2021imetoka Shilingi bilioni 32 ambazo zimetumika kwenye miradi ya utafiti na ubunifu.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko amemsema hayo Disemba 02, 2024 wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano la tisa la Sayansi, Teknolojia, Ubunifu na maonesho linaloendelea Jijini Dar es Salaam.
Amesema Serikali inatambua mchango wa wanasayansi na kuwawezesha watafiti na wabunifu na kupitia Tume  ya Sayansi na Teknolojia COSTECH imetoa kiasi cha bilioni 32 kwa ajili ya kuimarisha miradi ya utafiti na ubunifu katika sekta Zaidi ya 20 ikiwemo afya, elimu, nishati na kilimo.

“Umefika wakati kwa Serikali na taasisi na mashirika kutambua, kuthamini na kutumia tafiti za wanasayansi wa ndani ya nchi ili kutatua changamoto zilizopo,” amesema Dkt. Biteko.

Dkt. Biteko amesema wanasayansi nchini wanafanya kazi nzuri na kubwa ya kutafuta suluhu ya matatizo mbalimbali katika jamii lakini kazi zao zinatambuliwa zaidi nje ya nchi kuliko zinavyotambuliwa nchini jambo ambalo linaweza kuwavunja moyo.

“Kongamano hilo ni la kujadili na kutafuta suluhu ya matatizo tuliyonayo, tutumie tafiti za wanasayansi wa ndani badala ya kuwavunja moyo na kila anayejaribu kwa kutafiti apewe fursa ili aendelee kutafiti zaidi na matokeo tutayaona,” amesema DKt. Biteko.

Tangu mwaka 2015 Serikali imeshapokea kiasi cha shilingi bilioni 222.8 kwa ajili ya kujenga uwezo kwa wanasayansi wabunifu kuendeleza miradi mbalimbali ambazo zimesaidia kuwajengea uwezo wanasayansi wakiwemo wanasayansi vijana.

Naye Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia. Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali imeanza kutambua jitihada za Wanasayansi, Watafiti wa ndani ya nchi na baadhi yao wametunukiwa vyeti kwa kutambua mchango wao kwa maendeleo yaliyofikiwa katika sekta mbalimbali ikiwemo Afya, Kilimo na Uvuvi.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia. Prof. Adolf Mkenda.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter