Home BIASHARAUWEKEZAJI Bandari kavu ya Kwala yaleta mapinduzi sekta ya uchukuzi

Bandari kavu ya Kwala yaleta mapinduzi sekta ya uchukuzi

0 comment 32 views

Uwepo wa Bandari Kavu ya Kwala katika eneo la Vigwaza, Mkoa wa Pwani, umeleta mapinduzi makubwa katika sekta ya uchukuzi.

Kutokana na mapinduzi hayo, msongamano wa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam umepungua na kurahisisha usafirishaji wa shehena kupitia reli na barabara kuu.

Hayo yameelezwa Machi 16, 2025 na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika bandari hiyo.

Msigwa amebainisha kuwa Bandari Kavu ya Kwala tayari imepokea makontena 700, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita kuboresha miundombinu na kuimarisha biashara.

Mbali na mafanikio hayo, Msigwa pia ameupongeza Mkoa wa Pwani kwa mafanikio makubwa katika sekta ya viwanda, ambapo chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa Abubakar Kunenge, mkoa huo umepokea miradi 369 ya uwekezaji, ikiwa ni pamoja na viwanda 247 vyenye uwekezaji wa jumla ya Dola Bilioni 4.6 (zaidi ya Shilingi Trilioni 11).

Sekta ya viwanda pekee inachangia Dola Bilioni 2.8, ikithibitisha kuwa Mkoa wa Pwani ni kitovu cha maendeleo ya viwanda nchini.

Kuhusu Kongani ya Viwanda ya Sinotan, yenye ekari 2,500, Msigwa alieleza kuwa mradi huu wa Dola Milioni 327 unatekelezwa kwa awamu tano, ukitarajiwa kuwa na viwanda vikubwa 200 na vidogo 300.

“Awamu ya kwanza tayari imekamilika kwa asilimia 80, huku mradi ukitarajiwa kutoa ajira 100,000 za moja kwa moja na 500,000 zisizo za moja kwa moja.

Maendeleo haya yanadhihirisha dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuimarisha mazingira ya uwekezaji, kukuza uchumi wa viwanda na kuboresha miundombinu ya nchi kwa ujumla,” ameeleza Msigwa.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter