Home KILIMO Faida za kulima mbogamboga

Faida za kulima mbogamboga

0 comment 162 views

Umeshawahi kufikiria kuingia katika shughuli za kilimo? Vijana wengi hapa nchini hivi sasa wamekuwa wakijishughulisha na masuala ya kilimo kama njia mojawapo ya kujiajiri na pia kutoa ajira kwa wengine. Kilimo cha mbogamboga kimekuwa kikipata umaarufu hapa nchini na watu wengi zaidi wamekuwa wakijiajiri kupitia kilimo hicho. Zifuatazo ni baadhi ya sababu kwanini kilimo cha mbogamboga ni fursa nzuri kwa vijana.

Kilimo hichi huitaji mtaji mdogo tu. Kilimo cha mbogamboga kinaweza kuanza katika eneo dogo hivyo gharama za kuendesha zinakuwa chini. Bustani inaweza kuanzishwa nyumbani katika eneo dogo na mkulima anapaswa kuhakikisha kuwa upatikanaji wa maji na mbolea ni wa uhakika. Pia inatakiwa kupulizia dawa kuhakikisha wadudu hawaharibu mboga. Ni kiasi kidogo tu cha fedha kinahitajika ili kujishughulisha na aina hii ya kilimo.

Kilimo cha mbogamboga ni njia nzuri ya kujiajiri. Baada ya kupoteza muda mwingi kuhangaika kutafuta kazi. Kilimo hiki ni njia mbadala kujiajiri na kujiingizia kipato. Hakihitaji gharama kubwa hivyo inakuwa rahisi zaidi kujiajiri. Pia inawezekana kujiunga katika vikundi na kuwa wengi ili kuzalisha zaidi na kujiongezea kipato. Hivyo vijana watumie fursa hii kujiajiri na kujiingizia kipato.

Kilimo hiki hakichukui muda mrefu kuonyesha mafanikio. Mbogamboga huchukua muda mfupi hivyo fedha utakazopata katika biashara hii zinaweza kutumika katika shughuli nyingine za maendeleo na hivyo mbogamboga ni sekta nzuri ya kuwekeza. Fedha ambazo utazipata zinaweza kutumika kuwekeza katika mambo mengine na kujiweka katika nafasi nzuri zaidi kiuchumi.

Vijana wajifunze aina hii ya kilimo ili wajiweke katika nafasi nzuri zaidi ya kujikwamua na umaskini. Kilimo cha mbogamboga mbali na kuwa na faida kubwa pia kinawasaidia vijana wengi kujitegemea kifedha hivyo kujiweka katika nafasi nzuri kiuchumi. Mashirika na taasisi za serikali pamoja na zile zisizo za serikali ziendelee kushirikiana na wakulima wadogo ili kuwasaidia kuwainua wakulima hao.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter