Baada ya kutembelea kituo cha kupoza umeme cha Zuzu mkoani Dodoma, Rais wa Benki ya Maendeleo ta Afrika (AfDB) Dk. Akinumwi Adesina amesema benki hiyo imeridhishwa na mwenendo wa mradi huo pamoja na miradi ya nishati kwa ujumla hapa nchini.
Dk. Adesina amesema mbali na benki hiyo kutambua jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kuleta maendeleo hususani katika kuboresha sekta ya nishati ambayo ni muhimu kwa wananchi, AfDB pia imetoa Dola za Marekani milioni 75 ili kufanikisha ujenzi wa kituo hicho ambacho thamani yake ni zaidi ya Dola za Marekani milioni 220.
Dk. Adesina ameeleza kuwa mradi huo unalenga kupunguza changamoto ya upatikanaji wa umeme kwa watanzania na vilevile katika nchi jirani za Kenya na Burundi.