Home KILIMO ASDP II haitofanikiwa bila vijana

ASDP II haitofanikiwa bila vijana

0 comment 105 views

Siku chache baada ya Rais John Magufuli kuzindua Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP II), baadhi ya wadau kutoka asasi za kiraia wamedai endapo serikali haitojipanga vizuri kurekebisha kasoro zilizopita, changamoto za programu hiyo kwa awamu ya kwanza zinaweza kujirudia.

Wadau hao wameitaka serikali kuwa makini na kushirikisha makundi husika. Akizungumzia programu hiyo, Katibu Mtendaji wa Jukwaa la Kilimo la Asasi za Kiraia (Ansaf) Audax Rukonge amesema ili mpango wa sasa ufanikiwe, ni lazima wananchi hasa vijana washirikishwe.

Ameongeza kuwa japokuwa ajira za maofisa ugani zinapatikana, kumekuwa na ukosefu wa vitendea kazi pamoja na rasilimali fedha hivyo hata utendaji wa kazi umekuwa hafifu.

Kwa upande wake, Mtafiti wa ardhi na kilimo Emmanuel Sule amesisitiza kuwa mpango uliopo hauna tatizo bali ugumu unakuja kwenye utekelezaji. Ameeleza mipango mingi ambayo ilikuwepo hapo awali kama vile Mpango wa Siasa ni Kilimo (1972), Kilimo cha Kufa na Kupona (1983) na Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) wa mwaka 2006 ambao baadae ulibadilishwa na kuhamia kwenye Mpango wa Kilimo Kwanza.

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter