Home FEDHA Fedha kutopelekwa mifuko maalum kwaibua maswali

Fedha kutopelekwa mifuko maalum kwaibua maswali

0 comment 100 views

Kamati ya Bajeti imehoji kuhusu Sh. 755.29 bilioni zilizokusanywa na serikali lakini hazikupelekwa kwenye mifuko maalum iliyoanzishwa na serikali kwa ajili ya mikakati ya umeme, maji, reli na miradi ya barabara.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hawa Ghasia ameeleza kuwa fedha hizo zina uzio wa kisheria na hazipaswi kuwekwa katika mfuko wa serikali.

Mbali na hayo, Kamati ya Bajeti pia imetoa wito kwa Bunge kuishauri serikali kutoingilia mifuko hiyo kwani kufanya hivyo kunaathiri ufanisi.

Kati ya fedha hizo, Sh. 273.89 bilioni zilikusanywa kama ushuru wa maendeleo ya reli lakini hazikufika katika miradi iliyokusudiwa.

Katika uchambuzi uliofanywa na kamati hiyo kwenye mfuko wa barabara unaokusanya mapato kutokana na ushuru wa magari ya kigeni mpakani, tozo za mafuta ya petrol, dizeli pamoja na magari yanayozidisha uzito, uliidhinishwa Sh.917.548 bilioni mwaka 2017/2018 lakini kufikia Aprili, asilimia 68.5 ya fedha hizo zilikuwa zimekusanywa na Wizara ya Fedha na Mipango.

Ghasia ameshauri Bunge kupewa taarifa ya makusanyo na utolewaji wa fedha hizo kwa Mei na Juni ili mfuko huo uweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu

About Us

PesaTu ni kitengo cha habari cha MediaPix ambacho huandika makala za biashara na uchumi wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Waasisi wa kampuni wana uzoefu mkubwa kwenye tasnia ya habari na mawasiliano wakiwa kwenye fani hio tangu mwaka 1905.

Editors' Picks

Newsletter