Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Ladislaus Matindi amesema hivi sasa shirika hilo linaendesha utafiti katika viwanja vya ndege vya mikoa ya Tanga, Musoma, Iringa, Shinyanga, na wilaya na Mpanda mkoani Rukwa ili kuandaa mazingira ya kuanzisha safari katika mikoa hiyo na kutoa nafasi kwa watanzania wote kunufaika na huduma za usafiri wa anga.
Mbali na kufanya hivyo, Mashindi pia amedai kuwa ATCL inajipanga kuongeza safari kwenye baadhi ya mikoa kama Dodoma.
Mkurugenzi huyo pia amezungumzia ndege mpya iliyowasili nchini siku chache zilizopita ya Boeing 787-8 Dreamliner an kusema kuwa, mafubani wote nane wa ndege hiyo ni watanzania na tayari wameshapatiwa mafunzo. Safari ya kwanza ya ndege hiyo inatarajiwa kuanzia jijini Dar es salaam kwenda Mwanza kupitia Kilimanjaro.